Maandamano yazidi Iran kisa kutokuwepo kwa mawasiliano ya mtandao

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Kilichoanza Novemba 15 mwaka huu kama mfululizo wa maandamano ni kupinga kupanda kwa gharama za mafuta yaliyosababisha mashinikizo ya kubadili utawala nchini Iran.

Raia wa Iran waliingia mitaani wakiwa wamebeba mabango ya kiongozi wa juu wa nchi hiyo, wakimuita dikteta.

Siku sita za maandamano katika miji mbalimbali ya nchi, kufungwa kwa mawasiliano ya intaneti kulisababisha watu 106 kuuawa, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa na Shirika la mnesty International, ingawa vyanzo vingine vimesema idadi ya waliopoteza maisha inaweza kuwa kubwa zaidi.

Iran imethibitisha kuwepo kwa madhara kadhaa, na kuwashutumu watu waliowaita ''wanyang'anyi'' ikiwahusisha na maadui wa kigeni.

Ingawa maafisa wa Umoja wa Mataifa umezitaka mamlaka za Iran kutotumia silaha dhidi ya waandamanaji, picha za video zilionesha vikosi vya usalama vikiwafyatulia riasai waandamanaji.

Wafuatiliaji wa masuala hayo wamesema kuwa amri ya kudhibiti maandamano haikuwa na chembe ya huruma ambayo ilisababisha si tu mauaji na majeruhi lakini pia maelfu walikamatwa.

Wataalamu wameeleza kuwa maandamano haya hayakuwa tu mjini Tehran, bali nchi nzima, miji kadhaa midogo na mikubwa ilihusika.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad