'Mh Rais hali ni ngumu, achia pesa' - Mwananchi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mwanaume mmoja mkazi wa Igunga, mkoani Tabora, aliyejitambulisha kwa jina la Abel Mpinga, amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, kuachia pesa kwa kuwa sasa maisha yamezidi kuwa magumu, hali inayopelea akina Mama kunyang'anywa vifaa vyao kutokana na made

Ombi hilo amelitoa leo Novemba 27, 2019, wakati Rais Magufuli aliposimama njiani kuwasalimia wakazi wa Igunga, ambapo mwanachi huyo alidai kuwa hali ya maisha imezidi kuwa ngumu hivyo ni vyema sasa pesa ikaachiwa.

"Mheshimiwa kama itakupendeza maisha ni magumu sana, fedha hakuna, watu wana hali mbaya, akina Mama wananyang'anywa Tv, Friji kwa mikopo midogomidogo, tunaomba uachie fedha, mengine yote hatuna tatizo na wewe yakikamilika haya hata ukitawala milele sisi hatuna shida" amesema Abel.

Akijibu ombi hilo, Rais Magufuli amesisitiza umuhimu wa kila mtu kufanya kazi kwa bidii.

"Usipofanyakazi hela zitaisha tu ni kweli wapo wanawake wenye pesa wanaoenda kuposa wanaume, sasa anayeoa mwanamke au mwanaume? cha bure hakipo hata mimi sina, kinachotakiwa ni kuchapa kazi, wewe ukitaka pesa nenda hata kwenye machimbo, mimi sikuja kuleta hela nimekuja kuwaambia mfanye kazi" amesema Rais Mgufuli.



----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad