11/12/2019

Vurugu Alizofanya EBITOKE Mkutano wa Mlela...Meneja wa Hotel Adai ni Mpango Ulipangwa..Umesababisha Hasara Kubwa

Taarifa nyingine imeibuka baada ya Muigizaji **Ebitoke kusababisha vurugu kwenye mkutano wa Muigizaji Yusuph Mlela na waandishi wa habari uliofanyika leo Novemba 11 katika hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam.

Baada tukio hilo, alifuatwa Meneja wa hoteli hiyo, aliyejitambulisha kwa jina Suleiman Victor, ambaye alieleza kuwepo kwa mpango uliohisiwa kuhusishwa na tukio hilo lililosababisha hasara na uharibifu wa vitu kadhaa.

Meneja Suleiman alieleza kuwa Novemba 10, Mlela afika katika ofisi za hoteli hilo na kufanya
‘Booking’ kwa ajili ya mkutano huo na katika mazungumzo ya hapa na pale alinukuliwa katika maelezo kuwa kuna mchezo wataufanya.


Victor amesema Ebitoke alifika mapema na gari ambalo lilimuondoa eneo hilo na hawakupishana na kuwasili kwa kina Mlela.

Hata hivyo, baada ya kina Mlela kushuka na kuingia kwenye mkutano Ebitoke yeye alibaki kwenye gari hilo na dereva ambaye ni mwalimu wao wa mazoezi yeye na Mlela anayeitwa Denzel Condrad.

"Mkutano ukiwa unaendelea ndani, kaka mmoja aliyevaa kaptura nyeusi  ambaye ndiye alikuwa akiratibu mkutano akaenda kumchukua Ebitoke.

"Ghafla tukaona watu wanapigana huko ndani ya ukumbi na sisi kuja ili wasituharibie mali zetu lakini baadaye Mlela tulizungumza na akanitaarifu kuwa ndio drama aliyenieleza jana hapo naye hakutegemea kama ingekuwa hivyo," amebainisha Meneja huyo

Hata hivyo mpaka sasa haijabainika kama mpango huo ulilenga kufanyika kwa tukio hilo la vurungu inagwa katika maelezo ya juu juu, Yusuph Mlela alidai kuwa hakutegemea kama Ebitoke angefanya vurugu hizo.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger