Ujerumani Yaikosoa Marekani Kwa Kuingilia Mambo Yake ya Ndani....Urusi, Umoja wa Ulaya Nazo Zatoa Tamko

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Ujerumani imeishutumu Marekani kwa kuingilia masuala yake ya ndani katika matamshi ya hasira  kuhusiana na uamuzi wa Marekani kuweka vikwazo dhidi ya makampuni yanayohusika na mradi wa kusambaza gesi ya Urusi

Urusi  na  Umoja  wa  Ulaya  pia zimetoa taarifa  zinazokosoa vikwazo  hivyo, siku  moja  baada  ya  rais  wa  Marekani Donald Trump  kutia  saini  kuwa  sheria  hatua  ya  kuzuia  mali  na upatikanaji  wa  visa  kwa  wale  wanaohusika  katika  mradi  huo  wa Nord Stream 2.

Wabunge  wa  Marekani wanataka kuzuia  kile  wanachokiona kuwa  ni  ongezeko la  utegemezi wa  nishati  kutoka  Urusi  katika mataifa  ya  Ulaya  magharibi kwa  kulenga mradi  huo, ambao  una lengo  la  kuongeza  maradufu usambazaji wa  gesi  asilia  kutoka Urusi  nchini  Ujerumani  kupitia  katika  bomba  lililowekwa  chini  ya bahari ya  Baltiki.

Vikwazo  hivyo  vinalenga  wakandarasi wanaofanyakazi  katika kutandika  bomba  hilo  la  Nord Stream 2, mradi  wenye  thamani  ya euro  bilioni 10 unaotarajiwa  kukamilika  mapema  mwaka  2020, na mradi  mwingine  wa  gesi  wa  Urusi , unaojulikana  kama TurkStream.

Licha  ya  kuwa  bunge  la  Marekani waliunga  mkono  kwa  kiasi kikubwa  vikwazo, kulikuwa  na  baadhi  wamekosoa  hatua  hiyo ambayo  kimsingi  inawaadhibu  washirika  wa  NATO  kama Ujerumani.

Wakati msemaji  wa  Umoja  wa  Ulaya  amekosoa kile  alichokiita "uwekaji  wa  vikwazo dhidi  ya  makampuni  ya  Umoja  wa  Ulaya yanayofanyakazi  halali", serikali  ya  Ujerumani  imesema  Berlin inakataa "aina hii  ya  vikwazo dhidi  ya mataifa  ya  kanda".

"Hatua hii  itayaathiri   makampuni  ya  Ujerumani  na  Umoja  wa Ulaya  na  kufikia  katika  uingiliaji  wa  masuala  yetu  ya  ndani," amesema  msemaji  wa  kansela  Angela  Merkel , Ulrike Demmer.

Msemaji  wa  wizara  ya  mambo  ya  kigeni  ya  Urusi  Maria Zakharova  ameishutumu  Marekani  kwa  kuendeleza  nadharia ambazo  zinazuia  biashara  ya  dunia, na  kuongeza  katika ukurasa  wake  wa  Facebook: "Hivi  karibuni  watadai  kuwa  tuache kupumua."

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad