Benki ya Dunia yaahirisha kupigia kura ya Kuipa Mkopo wa Elimu Tanzania

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa


Benki ya Dunia imeahirisha kupiga kura kuhusu mkopo wa dola milioni 500 kwa Tanzania zilizokuwa zikilenga miradi mbalimbali ya elimu.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa BBC, Kura hiyo ilikuwa inatarajiwa kupigwa leo, lakini tayari kulikuwa na mgawanyiko mkubwa wa maoni juu ya benki hiyo iidhinishe mkopo huo kwa Tanzania ama la.

Taarifa za kuahirishwa kwa kura hiyo imekuja siku chache baada ya shinikizo kutoka kwa wanaharakati wa Tanzania na wa kimataifa waliokuwa wakiitaka benki hiyo isitoe mkopo huo kwa serikali kutokana na kile walichokiita kuwa ni sera na sheria ya elimu ya kibaguzi.

Kwa mujibu wa nyaraka za Benki ya Dunia, pamoja na mambo mengine, mkopo huu ulikusudiwa kwenda kusaidia upatikanaji wa elimu bora na kwa urahisi kwa wanafunzi waliokuwa wanarudi shule baada ya kuwa wamepata ujauzito.
 
Lakini mradi huu wa elimu ulikuwa ni kupitia elimu mbadala na si katika mfumo rasmi.

Kipengele ndicho kinachozua utata kiliwasukuma wanaharakati wa Tanzania kuiandikia bodi ya utendaji ya Benki ya Dunia ikiwa benki hiyo itaipa Tanzania mkopo huo, kabla ya nchi hiyo haijaahidi kuondoa sera na kipengele cha sheria kinachowakataza wanafunzi wa kike kurudi shuleni baada ya kujifungua, basi benki itakuwa imekubaliana na sera na sheria hiyo ambayo wanaharakati wanaiita ya kibaguzi.

Shirika la habari la CNN la nchini Marekani, limesema hakuna sababu rasmi iliyotolewa kuhusu kuahirishwa kwa kura hiyo japo inaripotiwa kuwa uongozi wa benki hiyo ulifanya kikao cha dharura na wanaharakati wa haki za binaadamu kutoka Tanzania na mashirika ya kimataifa jana Jumatatu.

The World Bank has postponed its decision on granting Tanzania a $500 million loan, following pressure from activists who oppose the country's policy of banning pregnant girls and young mothers from attending state school https://t.co/iirUVDqR2i
— CNN International (@cnni) January 27, 2020

_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad