Mada ya Leo ..Je..Ngono Ndiyo Silaha ya Mapenzi?...!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


KARIBUNI wapenzi wasomaji wa safu hii ya mahusiano ambayo huwajia kila Jumanne na Jumamosi, ikilenga kufahamishana hili au lile kuhusiana na mambo ya mapenzi, wengine wakiita mahaba.

 nigeukie mada ya leo ambayo inajadili suala zima la uhusiano baina ya ngono na mapenzi ambayo ilianzia Jumamosi iliyopita.

Leo nimewaletea maoni ya wasomaji wangu kuhusiana na mada hiyo kama ifuatavyo:

 Juliana  Mgulu wa Same, Kilimanjaro:  Kwa upande wangu, siamini kuwa ngono ni silaha ya mapenzi na kamwe sitaamini kwasababu  muhimu mi naelewa ilo tendo la ndoa si tendo la wachumba, mi nimesimama katika imani na mbona niko katika mahusiano muda mrefu na ninafurahia uhusiano wangu.

Rama wa Kimara kwa Komba, Dar es Salaam: Kwangu ngono ndoyo silaha ya mapenzi.

Doa Vitras wa Dar es Salaam: Unaweza ukawa na mwenzio na msifanye ngono na mambo yakawa sawa, siku zote ngono ni haja ya kimwili na si ugonjwa ukamfanya mtu akafa, mapenzi ni hisia na si matamanio ya mwili.

Mujuni wa Ubungo, Dar es Salaam: Kama mnapendana kwa dhati, tendo la ngono lazima ndio kiunganishi.

Nuru Shariff wa Tabata Matumbi, Dar es Salaam: Ngoni sio silaha ya kukupenda mtu. Hisia za mtu anayekupenda utazijua kwa vitendo vyake na si tabia. Ngono si mapenzi, wangapi wapo kwenye madanguro na kujirusha na watu, ina maana wanawapenda?

Bakari wa Kondoa: Ngono ni tendo lakini mapenzi ni zaidi ya ngono, kama wawili wana mapenzi toka moyoni, ngono si lolote si chochote. Ngoni ni sawa na kiu ya maji, ukinywa tu basi inakatika. Mapenzi ni mwili na roho.

Raymond Matenga: Kuwa na mwanamke au mpenzi anayekukatalia kufanya tendo la ngono eti mpaka muoane ni sawa na kusubiri meli uwanja wa ndege.

Maleck wa Sinza, Dar es Salaam: Mtu mwenye mapenzi ya kweli atakuwa tayari kwa chochote kwa mwenza wake kama anakuwa hataki, basi ujue anaye wake sio wewe. Ukiangalia hali ya sasa huwezi ukawa unamuhudumia mwenzio halafu haja zako hakutimizii, huyo hakufai.

Atambue kuwa manjonjo yake na mahaba atakayonifanyia tukiwa faragha, ndio zitanifanya name ninogewe nimng’ang’anie. Sasa kama hataki nitajuaje kuwa ni mwanamke aliyekamilika? Au atanijuaje kuwa mume aliyenaye yupo sawa? Aliye na malengo nawe  atakufanyia utakavyomuomba.

Tatizo la madada zetu wa siku hizi wana tamaa sana, pesa mbele kuliko utu ndio maana kuna anayemfaidisha kimwili na wengine wa kuwachuna. Hata mimi nimeachana na mwenzangu kwa jambo hilo, hataki kukutana na mimi kila muda ni mtu ambaye hana muda, siwezi kutoka.

 By Lydia wa Same, Kilimanjaro: Ngono sio silaha ya mapenzi kinachotakiwa ni upendo wa dhati, kama mtu hujampenda kutoka moyoni ni bora ukamwambia kuliko kumpotezea muda.

Baba Rooney wa Mbalizi Mbeya: Si kweli kuwa mpenzi ambaye hakupi mapenzi ndio hana mapenzi na wewe. Mbona wapo ambao anakupa mapenzi lakini hana maepnzi na wewe?

Sylvia Lucas wa Maduka Tisa, Mwanza: Ni kweli mtu akikataa kukutana kimwili huyo hakupendi, yupo anayempenda anakupotezea muda tu.

Athanas K wa Mbande, Dodoma: Ngono ni silaha kubwa katika mahusiano na ndio msingi wa halisi wa mapenzi kwa wawili waliokubaliana.

Wewe unamoani gani?tafadhali tuandikie hapo chini ,zingatia lugha nzuri
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mapenzi yana nafasi yake na ngono inanafasi yake na inategemeana na mahusiano yanu katika misingi ya imani yako kwa ufupi ngono ni kiunganishi cha upendo yani kamasawa na umepika mchicha bila chumvi sidhani kama utakunywa

    ReplyDelete
  2. Kama mpenzi wako anakuita mpenzi lakini hakupi tamu yake ujuwe wewe ni "mpenzi mtazamaji"

    ReplyDelete
  3. Mpenzi wako anakuita mpenzi na hakupi tamu yake basis ujuwe wewe ni "mpenzi mtazamaji"

    ReplyDelete
  4. Kuna mwanaume mmoja alisema hataki kufanya mapenzi hadi wafunge ndoa kilichotokea jamaa alienda kumsalimia mwenzake dar akakuta ana mimba ya mwezi na alipoulizwa akajibu eti alihisi mwenzake jogoo hawiki.Mungu atusaidie Sana wanaume.

    ReplyDelete

Top Post Ad