AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Mataifa yaliyopoteza raia katika ajali ya ndege ya Ukraine iliyodunguliwa na Iran yameitaka Tehran iwajibike kikamilifu, uchunguzi wa kimataifa uanzishwe na familia za wahanga zilipwe fidia.
Mawaziri wa mambo ya nje wa Canada, Uingereza, Ukraine, Sweden, Uholanzi na Afghanistan wamekutana jijini London katika ubolozi wa Canada.
Mawaziri hao baada ya mkutano wao walitoa taarifa ya pamoja wakiitaka Iran ifanye uchunguzi wa kimataifa utakao kuwa huru na wazi hasa kwa mataifa yanayoomboleza.
Waziri wa mambo ya nje wa Canada Francois-Philippe Champagne amesema wamekutana kutafuta uwajibikaji na haki kwa wahanga wa mkasa huo na kuongeza kuwa familia za wahanga hao zinataka majibu, jamii ya kimataifa inataka majibu na dunia nzima pia inasubiri majibu na kwamba hawatapumzika hadi watakapoyapata.
Watu wote 176 waliokuwa ndani ya ndege ya abiria ya Ukraine walipoteza maisha yao wakati ndege yao ilipodunguliwa na kombora muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Imam Khomeini mjini Tehran tarehe 8 mwezi huu.
Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu
Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK