Dudu Baya asamehewa kifungo chake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Serikali ya Tanzania imemsamehe msanii, Godfrey Tumaini maarufu Dudubaya baada ya kumfungia kwa muda usiojulikana kujihusisha na kazi za sanaa. Alifungiwa na Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) baada ya kukataa wito kuhojiwa kuhusu tuhuma alizozitoa katika mitandao ya kijamii kuhusu sanaa. Baraza hilo limeeleza kuwa Dudubaya alitumia lugha zisizo na maadili.



Hata hivyo, Januari 23, 2020 Dudubaya alijisalimisha Basata na kuomba msamaha lakini baraza hilo halikutoa uamuzi wowote kwa kuwa mamlaka ya kufanya hivyo ipo chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Jana Jumanne Februari 11, 2020 msani huyo alikwenda katika ofisi za Waziri wa wizara hiyo, Dk Harrison Mwakyembe kuweka mambo sawa.

Leo Jumatano Februari 12, 2020 katibu mtendaji wa baraza hilo, Godfrey Mngereza amesema Dudubaya amesamehewa baada ya kusikilizwa na Dk Mwakyembe.

Amesema Basata haikuwa na mamlaka ya kumfungia na aliandika barua ya kukata rufaa kwa waziri, “sheria ya baraza namba 23 ya mwaka 1984 na marekebisho yake yaliyofanywa mwaka 2006 inaeleza mtu yeyote akipewa adhabu na Baraza, sheria inampa nafasi ya kwenda kumuona Waziri na anachosema Waziri ndicho kitakachotekelezwa.”

Mngereza amewataka wasanii kuzingatia sheria kanuni na taratibu, “wasanii wana nguvu kubwa, wanapaswa kuishi kwa kufuta maadili kwani watu wengi wanawafuatisha wakiwemo watoto, pia haileti picha nzuri katika sanaa ikizingatiwa kuwa ni moja ya kipengele kinachoitambulisha nchi.”

CHANZO: Mwananchi


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad