Gesi yalipuka wanahabari wajeruhiwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Waandishi wa habari wanne wa kampuni za Star Tv, Abood Media, Global Tv na Imani Media wamejeruhiwa na moto baada ya kulipuka kwa mitungi ya gesi kwenye moja ya nyumba mtaa wa Msamvu, manispaa ya Morogoro.

Wanahabari waliojeruhiwa ni Omary Hussein (Star Tv) aliyejeruhiwa mkononi; Hassan Ninga (Imani Media) na  Nicholas Mwanaharusi (Global Tv) waliojeruhiwa kila mmoja mguuni na Salum Yusuf (Abood Media) aliyejeruhiwa usoni, mikononi na miguu.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Wilbrod Mutafungwa amesema tukio hilo limetokea leo Jumamosi Machi 14, 2020 saa 9:00 alasiri maeneo ya Mafisa katika moja ya nyumba inayohifadhi mitungi ya gesi.

Amesema wanahabari hao walifika eneo la tukio kwa nia ya kuchukua habari baada ya kupata taarifa ya kuungua kwa nyumba hiyo.

Amebainisha kuwa baada ya kurekodi wakiwa wanaondoka eneo hilo, mitungi mingine ililipuka na kuwaunguza. Amesema hali zao zinaendelea vizuri huku mmiliki wa nyumba na muuza gesi wakitafutwa na polisi.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad