Mbowe Ajiweka Karantini Wakati Akisubiria Majibu yake ya Corona

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Mwenyekiti wa Chadema ambaye pia ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe ameamua kujiweka karantini na familia yake baada ya mtoto wake kukutwa na virusi vya corona.

Juzi Katika taarifa yake kwa umma, Mbowe alieleza kuwa  mtoto wake aitwaye Dudley amethibitika kupatikana na virusi vya corona baada ya kupata homa za vipindi, kuumwa kichwa mfululizo na kukohoa kwa siku tano.

Akizungumza jana machi 25. 2020  na Clouds FM katika kipindi cha Jahazi, Mbowe amesema baada ya taarifa hizo ameamua kujitenga peke yake nyumbani Dodoma ambapo anaendelea na shughuli zake huku akisubiri majibu ya vipimo alivyofanya ili kuthibitisha kama amepata virusi hivyo au hakupata.

Vilevile, Mbowe amesema mbali na yeye kujitenga lakini pia familia yake ambayo ilikuwa karibu na mtoto ambaye amekutwa na virusi hivyo nao wamejitenga kwa siku 14 kwa lengo la kuona kama wamepata virusi hivyo

“Nipo Dodoma lakini nimeamua kwenda kwenye self-Isolation kwa sababu ikishasemekana kuwa familia yako ina ugonjwa huo kila mtu anakuangalia kwa jicho la hofu, unaingiza hofu katika jamii hivyo nimeamua kujitenga kukaa nyumbani na kufanyia kazi zangu nyumbani nasubiri majibu yangu” ameeleza Mbowe
 
Mbowe amesema tangu akutane na mwanaye huyo mwenye virusi hivyo ni zaidi ya siku 12 ambao ni muda mrefu lakini baada ya kutoka nyumbani alitembelea maeneo mbalimbali na kukutana na watu wengi ambapo amesema ni jambo la kumuomba Mungu awe hajapata virusi hivyo ili na watu aliokutana nao wawe salama.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Pongezi kwa Mh Makonda.
    Tungeyajua haya.?

    Mtowe aliamua kuminya zaidi ya siku 9.

    Nia yako na Azumuni ni Aje..??

    Muuaji siyo msika kisu tu...!!

    Biswilo unaliangaliae swala hili..!!

    ReplyDelete

Top Post Ad