Je Kwa Mwanamke Ndoa Ndiyo Kila Kitu?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Katika makuzi yangu kama binti wa Kiafrika nimefunzwa mambo mengi kuhusu maisha na wajibu wangu kama mtoto wa kike.

Baada ya kuvunja ungo nilianza kuandaliwa kuwa mke mtarajiwa wa mwanaume nisiyemfahamu. 

Nimefunzwa kupika, nimefunzwa usafi wangu wa mwili, nimefunzwa usafi wa nyumba, nimefunzwa kuvumilia maisha ya ndoa na nikaaminishwa kwamba mwanaume ndiye kichwa cha nyumba na nikafunzwa wajibu wangu katika kumtumikia, lakini pia nikafunzwa kupanga bajeti na kuweka akiba ili huyu mume ambaye ni kichwa cha nyumba akikwama kupata mkate wa kila siku kwa ajili ya familia niweze kumsaidia.

Kwa kifupi ni kwamba nilifunzwa mambo mengi lakini yote hayo yakiniaminisha kwamba siku isiyo na jina lazima nitaolewa na kuwa chini ya mwanaume ambaye atakuwa ndiye kila kitu kwangu.

Nakumbuka wakati fulani baada ya mama kuona mabinti ambao nalingana nao umri na wengine nikiwa nimewazidi umri wakiolewa pale mtaani mama alianza kunidodosa kama sijapata mtu kama wenzangu.

Lakini pia alijaribu kutumia misamiati mbalimbali na mafumbo lakini nilielewa kwamba alikuwa anamaanisha nisiwe mgumu sana kwa wanaume kwani sijui aliyevutiwa na mimi na anayetaka kunioa. 

Nadhani alikuwa anataka kufikisha ujumbe kuwa umri unasonga na wenzangu wanaolewambona miye sisomeki?

Naamini si mimi peke yangu, ninayekabiliana na changamoto hizi za wazazi na jamii kwa ujumla.

Ukweli ni kwamba malezi ya mtoto wa kike yanamuandaa kuwa mke wa mtu, yanamuandaa kuolewa na yanamuaminisha kwamba ndoa ndiyo kila kitu.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mbona sasa mkishawekwa ndan mafundisho yote mnatia kapun mnakuwa jeuri? sasa mi nataka anayependa kweli tuoane nae na azngatie maadili,Jacky.

    ReplyDelete
  2. yeah ndoa ni kila kitu, ndoa ni stara, ndoa ni heshima, ndoa ni familiy, ndoa ni nusu ya dini.

    ReplyDelete
  3. mdau wa kwanza hapo juu, ndani ya nyumba ukujieshim utaeshimiwa,,, iyo ndo kanuni... Mtu aezi kuwa jeuri kama ujamchokoza

    ReplyDelete
  4. Mimi baba anajivunia kuwa na mabinti wote waliofunga ndoa.nimeshaona akijisifia kwa wenzake he is luck.

    ReplyDelete

Top Post Ad