Wachezaji marufuku kutema Mate uwanjani, kurejea kwa Premier League

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Wachezaji na Makocha wa Premier League hawatalazimika kuvaa barakoa uwanjani ligi hiyo pendwa itakapoanza kurejea tena baada ya kusimama mwezi Machi kufuatia mlipuko wa janga la virusi vya Corona.

Mbali na hilo klabu hizo zilikubaliana hapo jana siku ya Alhamisi kuwa wachezaji hawatatakiwa kutema mate uwanjani au kusafisha pua zao na kutokumbatiana wakati wa kushangilia magoli. Pia hakutakuwa na watoto wa kuwarushia wachezaji mipira inayotoka nje, na badala yake mfumo maalumu wa mipira iliyosafishwa utatumika.

Katika mchezo wa kwanza Watanzania wengi na wapenda soka duniani watakuwa wakiufuatilia mechi ya Aston Villa mabosi wa Mshambuliaji wa Tanzania Mbwana Samatta watakapo kabiliana na Sheffield United, Juni 17.

Hali hiyo ni tofauti na Bundesliga ambapo wao Ujerumani wachezaji, makocha wanatakiwa kuvaa barakoa muda wote isipokuwa muda wa mechi.

Katika ligi ya EPL hawatatakiwa kuvaa barakoa kabisa, hata katika vyumba vya kubadili na kwenye mabenchi ya makocha na wachezaji wa akiba. Hata hivyo, kamisaa wa mchezo na madaktari wa timu watatakiwa kuvaa barakoa.

Jana Alhamisi uongozi wa EPL ulitangaza kuwa kutakuwa na ukimya wa dakika moja katika mechi zote za awali kwa lengo ili kuwakumbuka wale wote waliopoteza maisha katika janga hili.

Beji maalumu za umbo la kopa zitavaliwa na wachezaji kwa lengo la kuwashukuru wahudumu wa Afya na wafanyazi wengine waliokuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya corona.

Klabu za EPL zimekubaliana pia kuhusu kanuni kadhaa za kiafya ambazo zitatekelezwa kwenye mechi zote zijazo. Idadi ya watakaoruhusiwa uwanjani itadhibitiwa na viwanja vitagawiwa katika maeneo maalumu ili kuzuia mchangamano usio wa lazima.

Kwa ujumla, watu wataotakiwa kuwepo uwanjani hawatazidi 300 na katika ‘eneo jekundu’ hawatatakiwa kuzidi 110 ikiwemo wachezaji na maafisa wa klabu. Kutafanyika usafi wa hali ya juu wa maeneo ya vibendera vya kona, milingoti ya magoli, vibao vya kubali wachezaji na mipira kabla na baada ya kila mechi.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad