Kasesela awaomba radhi wakazi wa Iringa aliowakosea

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



 
Dar es Salaam. Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amewaomba radhi  wakazi wa wilaya hiyo aliowakosea katika kipindi cha utawala wake.
Kasesela ametoa kauli hiyo siku moja baada ya kutemwa kwenye nafasi hiyo kutokana na uteuzi wa wakuu wa Wilaya uliofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan jana, Jumamosi Juni 19, 2021.

Mwanasiasa huyo ameomba radhi wakazi hao kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram ambapo ameandika ifuatavyo; "Wana-Iringa imekuwa furaha kufanya kazi na nyie mmejenga mahusiano makubwa na udugu nitaendelea kuwakumbuka sana,

"Nawashukuru viongozi wangu niombe radhi kwa wale niliowakosea haikuwa kwa nia mbaya, upendo ndio msingi wa maisha"amesema

Katika uteuzi alioufanya Rais Samia, Mohamed Hassan Moyo ndiye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa akirithi mikoba iliyoachwa na Kasesela.


 
Kasesela ni miongoni mwa viongozi waliokuwa wanashutumiwa na wananchi  kutumia vibaya madaraka ikiwemo kutoa maneno ya kejeli hasa kwa wapinzani.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad