Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

John Bocco: Simba SC wananidai makombe matatu
MSHAMBULIAJI na Nahodha wa Simba, John Bocco, ameweka wazi kuwa licha ya kufanikiwa kutwaa makombe manne mfululizo ya Ligi Kuu Bara, bado ana deni la mataji matatu ili kufikisha saba.

 

Leo Jumapili, Simba inatarajiwa kukabidhiwa rasmi kombe lao la Ligi Kuu Bara kwa msimu huu wa 2020/21, ambalo wamelitwaa mara nne mfululizo.

 

Zoezi hilo litafanyika baada ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo utakaopigwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

 

Akizungumzia mafanikio yao msimu huu, Bocco alisema: “Kwanza tunamshukuru Mungu kwa kufanikiwa kutwaa ubingwa wetu wa nne mfululizo, hakika haikuwa kazi rahisi kwetu na mashabiki wetu, hivyo kila mmoja anastahili pongezi kubwa kwa mafanikio haya.“

 

Lakini licha ya mafanikio haya, binafsi najiona kuna deni kubwa mbele ya Wanasimba la kuendeleza utawala wa kutwaa makombe zaidi, natamani kuona tukitwaa angalau makombe saba mfululizo, lakini pia natamani kuona tunawapa Wanasimba Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika.”

STORI: JOEL THOMAS, DAR

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments