Majaliwa Aipa Siku Saba Tume Kuchunguza Chanzo Cha Moto Soko La Kariakoo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Waziri Mkuu Kaasim Majaliwa ameipa siku saba za awali tume aliyoiunda kuchunguza chanzo cha moto katika soko la kimataifa la Kariakoo ili kubaini nini kimesababisha au nani kasababisha moto huo.

Ametoa kauli leo (Jumapili Julai 11, 2021) alipokuwa anaongea na wafanyabiashara na wakazi wa eneo la Kariakoo baada ya kukagua hatua zinazoendela kuchukuliwa kudhibiti moto huo, Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa kamati iliyoundwa ambayo itafanya kazi na kamati ya ulinzi na usalama iliyoanza kufanya kazi chini ya Mkuu wa Mkoa huo itajumuisha Ofisi ya Rais-Ikulu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo itawakilishwa na Mkurugenzi wa Maafa.

Wengine ni Vyombo vya Ulinzi na Usalama ikujumuisha Jeshi la Wananchi, Jeshi la Polisi, Zimamoto pamoja na Taasisi ya Kupambana na Rushwa. Pia Waziri Mkuu alizitaja Wakala wa Majengo, Shirika la Umeme (TANESCO), Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP)

“ Endapo itagundulika kama kuna mtu alihusika kwa namna moja au nyingine, hatua kali za kisheria zitachukuliwa moja kwa moja, kitendo cha kuungua kwa soko hili la miaka chungu mzima lazima kuwe na uchunguzi wa kina, kwanini leo lishike moto”

Aidha, Waziri Mkuu amewataka wafanyabiashara katika soko hilo wawe watulivu wakati Serikali inafanya kazi yake ya kujua chanzo cha moto huo na amewahakikishia usalama wa mali zilizo ndani ya soko hilo

Waziri Mkuu pia aliwataka wafanyabiashara kutoingia ndani ya soko hilo katika kipindi hiki ambacho udhibiti unaendelea hadi pale timu zilizoundwa zitakapojiridhisha na utulivu na kufanya sensa ya watu wenye mali kuingia mmoja baada ya mwingine ili wakatoe vitu walivyoviacha

“Tunachoshukuru kule chini shimoni hakuna moto, mali zote zinalindwa, msiwe na mashaka milango yote imefungwa na makamanda wako ndani na nje wanalinda, mali zote zimehifadhiwa, msiwe na mashaka”

Kadhalika Waziri Mkuu amewaahidi wafanyabiashara hao kuwa Serikali itaongea na Mabenki yaliyowakopesha wafanyabiashara waliounguliwa na mali zao kuwaongezea muda wa kulipa mikopo yao baada ya kuunguliwa.

“Tume itapata taarifa za kila mmoja mwenye mkopo rasmi kwenye taasisi za fedha ili tuzungumze nao waongeze muda waache kipindi hiki ili uweze kulipa hapo baadae utakapo kuwa umetulia,biashara imeungua naamini mabenki yatatuelewa na kuweka utaratibu mzuri”
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad