Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Mwijaku Ajitokeza na Kumtetea Barbara "Usisumbuke na Kelele za Wasio Jitambua"

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREMsanii wa Filamu na Mtangazaji, Mwijaku amesema yupo upande wa Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Barbara kwenye sakata lake dhidi ya Haji Marana.

Hiyo ni baada ya kusambaa kwa sauti za Manara mtandaoni akidai anashutumiwa na Barbara kuihujumu timu hiyo akidaiwa kukutana na viongozi wa Yanga maeneo ya Kariakoo na Kigamboni.

Sasa Mwijaku amemtaka Barbara kutosikiliza hayo maneno.

"Am so proud of you Barbara usisumbuke na kelele za wasio jitambua! Sisi wana Simba tunakuamini na tuko nyuma yako, hakuna mtu mkubwa zaidi ya Simba yenyewe".

"Na kama kuna wengine wanataka kuondoka waondokee tu na Kigoma wenye timu yetu tutakuwepo na tutashinda tu Wasemaji wa kujitolea tupo hapa, time to shine madam" amesema Mwijaku.

Kwa upande wake Barbara alipoulizwa mapema leo asubuhi amesema amesikia maneno hayo, lakini kwa sasa akili zake zipo kwenye mechi yao ya Fainali ya Kombe la ASFC dhidi ya watani wao, Yanga.

"Nimesikia hayo maneno, focus yangu kushinda mechi ya Jumapili, mengine yatafuata," amesema Barbara kwa ufupi.
-
Utakumbuka Simba na Yanga zitakutana kwenye mchezo huo wa fainali itakayochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika, mkoani Kigoma siku ya Jumapili.
-

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments