Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Harmonize Ahairisha Kumtoa Leo Msanii Wake Mpya Cheed


Kutoka kwa C.E.O wa @kondegang bwana @harmonize_tz ametangaza rasmi kusogezwa mbele kwa tarehe ya kuachia rasmi kazi za @officialcheed ambapo leo tarehe 24 ndio ilikuwa rasmi siku ya utambulisho wa kijana wake huyo ambapo walibatiza siku hii kwa jina la #CheedDay

@harmonize_tz hajasema rasmi kwamba lini itakuwa siku ya kuachiwa tena kwa kazi za @officialcheed Ila amesema taarifa itatolewa hivi karibuni..

MY TAKE: Binafsi toka akiwa @kingsmusicrecords Mimi nimekuwa namkubali saaana @officialcheed na ukweli hii siku nilisubiri kwa hamu kusikia package ya ngoma ambazo ametuandalia.

Ila naamini huenda kusogeza mbele kunatokana na maboresho makubwa ambayo yanatakiwa kufanyika binafsi nitaendelea kusubiri kwa hamu kusikia kazi hizo na utambulisho rasmi wa @officialcheed akiwa kwenye management mpya ya @kondegang

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments