Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Mange Kimambi Amshukia Ray C na Jack Wolper "Bila Mimi Kupost Video yako Ukiwa na Uraibu Usingefika Ikulu"
Miaka ya zamani kidogo kipindi ambacho kundi la muziki wa Bongo Flava, East Coast Team ambalo lilikuwa linaundwa na wasanii kama @aytanzania , @mwanafa , O ten, na mwanadada Legendary @jidejaydee likifanya vizuri, pia kulikuwepo na mwanadada mwenye sauti ya kipekee aliyekuwa moja ya wanaounda kundi hilo, Pauline Zongo ambaye video clip yake imekuwa ikitrend sana kwa sasa akioneka akiwa kachoka kwa uraibu wa madawa ya kulevya.

Wengi wamekuwa wakipost kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii akiwemo mwanadada, @mangekimambi_ kitu ambacho kuna baadhi ya mastaa kama @rayctanzania na @wolperstylish wamekichukulia kama ni udhalilishaji.

Mange hajataka kukubaliana nao wala kutaka kunyamaza,alichokifanya ni kuwajibu Ray C na Wolper kuwa👇

“Ray C na Wolper mmekosea kusema sikitakiwa kuposti video za Pauline Zongo au kwamba waliomchukua video wamekosea.

Ray C tena wewe ndo ulitakiwa ujue umuhimu wa hizi video kurushwa. Bila sisi kurusha video zako kipindi kile unadhani JK angekutafuta akusaidie. Ni hivi kuposti kwetu ndo kulikufikisha Ikulu, ni baada ya jamii kukuposti na kusikitika ndo JK akasikia kilio cha wananchi akakusaidia kwa niaba ya wananchi waliokuwa wanakuombea msaada.

Kwamimi kuposti habari za Pauline zitafika kwa mawaziri na hata kwa Rais.

Na sio hivyo tu hii itawaonyesha vijana wengine adhari za madawa ya kulevya.”

Kwako hii ishu unaionaje?


 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments