Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Simba: Subirini Muone Ukubwa Wetu

UONGOZI wa Simba, umeweka wazi kuwa, kuelekea Tamasha la Simba Day, Septemba 19, mwaka huu, wataonesha ukubwa wao kwa ajili ya mashabiki waliopo Tanzania na nje ya nchi.

Jumapili hii, Simba itafanya tamasha lao hilo la kila mwaka tangu kuanzishwa mwaka 2009 ambapo kilele chake kitahitimishwa kwa mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo.

Akizungumza na Spoti Xtra, Kaimu Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema kuwa mipango inakwenda sawa na wamejipanga kuwapa mambo mazuri mashabiki wao katika tamasha hilo.

“Maandalizi kwa ujumla yanakwenda vizuri, kikubwa ni kuona kwamba mashabiki wanaweza kujitokeza kwa wingi kushuhudia mambo mazuri ambayo tumewaandalia kwa ajili yao.

“Tumeona kwamba kumekuwa na muamko mkubwa kutoka kwa mashabiki, hilo lipo wazi na wapo wengine ambao watatoka nje ya nchi kwa ajili ya Tamasha la Simba, hivyo ni suala la kusubiri.

“Kwa wale ambao bado hawajapata tiketi muda ni sasa kwa kuwa tiketi zinapatikana, waje uwanjani tuwaoneshe ukubwa wa Simba ulivyo,” alisema Kamwaga.


 Downlaod App ya BLOG Hii Kutoka Google Play Kwa Kubonyeza HAPA>>>

Post a Comment

0 Comments