Mwanamuziki mashuhuri nchini Kelvin Kioko almaarufu kama Bahati amejipata pabaya mitandaoni baada ya kupakia video inayomuonyesha akijiburudisha na kuiambatanisha na ujumbe ambao wanamitando wengi wamehisi kwamba hauambatani kabisa na anachokifanya kwa video
Kwenye video hiyo ambayo amepakia kwenye ukurasa wake wa Instagram, Bahati anaonekana akivuta sigara inayowekwa kwa chupa maarufu kama 'Vape' huku akipiga densi kana kwamba anasherehekea. Kwa wakati huo mwanamuziki huyo ambaye tayari ametangaza kwamba amegura injili anaoekana akiwa amevalia mavazi ya kiarabu