Ticker

6/recent/ticker-posts

Album ya Alikiba inauzwa Kiholela Mtaani, Cosota Watoa Tamko Kali
Baada ya kuonekana album ya @officialalikiba THE ONLY ONE KING inauzwa kiholela mtaani na wale wanao bun CD pamoja na Flash kitu ambacho ni kinyume na sheria pia kutokuwepo makubaliano kati ya muhusika wa maudhui ambaye ni @officialalikiba pamoja na wauza CD pamoja na flash mtaani.

Siku ya jana wasimamizi wa kazi za wasanii @cosotatanzania wametoa tamko kwa wote wanaofanya hivyo mtaani kuwa kitendo hicho ni kinyume na sheria na adhabu yake ni faini ya mil. 20 au kifungo cha miaka mitatu mpaka mitano jela au vyote kwa pamoja.

Hivyo wamewatahadharisha kuwa wakiwa wanaendelea na taratibu za kuwafuatilia wauzaji wanatakiwa waache mara moja.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments