Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Hatimaye Drake Amiliki Rolls Royce Aliyokuwa Akiiikodi Kushow Off Kabla Hajatoka Kimuziki

HATIMAYE Staa wa muziki duniani, Aubrey Drake Graham maarufu kama Drake amefanikiwa kumiliki gari alilokuwa akilikodi kutoka kwa jamaa zake kwa takribani miaka kumi na nne (14) iliyopita, wakati akipambana kutafuta nafasi ya kufanikiwa kimuziki.


Drake sasa analimiki gari hilo baada ya meneja wake na Dj future the Prince, kuamua kumnunulia gari hilo aina ya Rolls Royce Phantom toleo la mwaka 2007 na kumpatia kama zawadi kwenye sherehe ya kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa.


Akizungumza kuhusu mapokezi yake juu ya zawadi hiyo, Drake alisema alikuwa akilikodi gari hilo kwa kiasi cha pesa Usd 5,000 ambazo ni sawa na 11.5 Milioni kwa mwezi ikiwa ni sehemu ya kuilinda hadhi yake na kutegeneza thamani yake mtaani katika kipindi alichokuwa akitafuta nafasi yakufikia malengo yake.


Rapa Drake kwa sasa ni mmoja wa wasanii wenye utajiri mkubwa akiwa anashikilia nafasi za juu kwenye chati mbali mbali za muziki Duniani.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments