Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Kimeumana..Mganga Aliyempa Uchawi Mchezaji Michael Essien wa Chelsea Kuwika Atangaza Kudhoofisha Kiwango Chake
Mganga wa jadi nchini Ghana ameibuka na kudai kwamba yeye ndio alisababisha mchezaji wa zamani wa @ChelseaFC, @MichaelEssien kushuka kiwango.

Mganga huyo wakati anafanya interview na mtangazaji Arnold Mensah Elavanyo katika kipindi cha Vibes in 5, alisema kwamba alishusha kiwango cha Essien baada ya kushindwa kutimiza ahadi zake ikiwemo ya kumnunulia nyumba katika mji wa Accra.


“Nimewatengeneza wachezaji 50 wa Ghana, na wengine bado wanacheza mpaka leo barani Ulaya. Essien alinipa ahadi ya kuninunulia nyumba katika mji mkuu wa Accra endapo nikimsaidia. Baada ya kufanikiwa akajisahau na mimi nikachukua maamuzi ya kumpoteza kabsa.”

Essien anatwaja kuwa moja kati ya wachezaji bora kuwahi kutokea barani Afrika, amecheza katika club kubwa kama Chelsea, Real Madrid na Ac Milan.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments