Ticker

6/recent/ticker-posts

Shaffih Dauda Awashukia TFF Kwa Kutomuweka Antonio Nugaz Tuzo za TFF "Amefanya Kazi Kubwa"
Nimeiona orodha ya wachezaji, wadau na viongozi wa mpira wa miguu kuelekea tuzo za TFF zitakazofanyika ukumbi wa JK Nyerere

Sina shaka na majina mengi kwenye vipengele vingi ila kwenye kipengele cha MHAMASISHAJI BORA nadhani hapo ndipo nina shida napo

Nimeona jina la Haji Manara, Masau Bwire na Bongo Zozo, YES wawili wa awali sina shida nao ila Hapo kwa BONGO ZOZO anaingia kama MHAMASISHAJI wa timu gani na ameajiriwa kwenye taasisi gani ya mpira wa miguu?

Pasi na shaka niliona nafasi ya Antonio Nugaz kwenye kipengele hicho kwa Kazi aliyoifanya pale Yanga, tena akitambulika kabisa kuwa ni Afisa Mhamasishaji, tunahitaji adubini kung’amua ukweli?

NUGAZ amefanya Kazi kubwa sana hata tukirejea kwenye takwimu za TPLB bado anasimama kwenye mzani wa peke yake na nafasi yake inaonekana Wazi, kwanini tumeificha kwa maksudi?

Sina shaka na ubora wa Bongo Zozo na mapenzi yake kwa mpira ila namuona Kama SHABIKI zaidi Kama Mashabiki wengine nchini ambao labda wangewekwa wote kwenye kipengele chao cha SHABIKI BORA

Namuona Bongo Zozo kama Issa Azam, Jimmy Kindoki, Aggy Daniel au Shabiki yoyote nchini ambaye anasafiri na timu yake kuipa nguvu binafsi nilimuona eneo hilo zaidi na sio Mhamasishaji

To be fair NUGAZ is robbed! Alipaswa kuwa hapo na alikuwa moja Kati ya washindi watarajiwa kwakuwa numbers don’t lie tena kwa takwimu zao wenyewe

Binafsi nimeitazama kwa mlengo huo zaidi

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments