Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Wimbo wa Msanii Camila Cabello Kutoka Cuba uitwao "Havana" Watunukiwa Tuzo ya Juu Duniani


Wimbo wa msanii @camila_cabello kutoka Cuba uitwao "Havana" uliotoka mwaka 2017 ambao kamshirikisha rappa Young Thug, umefanikiwa kuuza (units) 10,000,000 ambayo ni ngazi ya juu kabisa.

#Camila ambaye ni member wa kundi bora la muziki kuwahi kutokea ulimwenguni la @fiftyharmony, kutokana na hatua hiyo chama cha Recording Industry Association of America (RIAA) kimekabidhi tuzo maalumu (Plaque) maarufu kwa jina Almasi 💎 (Diamond).

@camila_cabello anakuwa msanii wa kwanza kutoka Cuba kufikia mafanikio hayo makubwa kupitia wimbo mmoja.

Lingine usilo lijua kuhusu "Havana" ni kuwa, rappa Young Thug ambaye ndiye kashirikishwa kwenye wimbo huo, hakutaka kutia verse yake katika havana kutokana na kutoielewa lakini kwa shinikizo la mama yake mzazi alifanya.

Kwenye mahojiano na #HipHopDX, Thug ameeleza kwamba hakuamini kama wimbo huo ungefanya vizuri kutokana na kuwa havikua vitu vyake lakini anafurahishwa kuona amekua moja ya watu walioshiriki katika wimbo huo ambao umetunukiwa tuzo maalumu (Plaque) ya Diamond na RIAA.

Na: @omaryramsey

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments