Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Familia ya Aliyeuawa na Polisi Kwa Kuchomwa Sindano ya Sumu Kulipwa Bil. 34/-

MAMLAKA za Jiji la Colorado zimethibitisha kuwa familia ya kijana aliyefariki baada ya kuchomwa sindano ya sumu na polisi italipwa fidia ya Dola za Marekani milioni 15 (zaidi ya Sh bil. 34 za Tanzania).

Elijah McClain mwenye umri wa miaka 23, alifariki mwaka 2019 mjini Aurora, ikiwa ni siku tatu tangu aliposimamishwa na polisi watatu na kisha kuchomwa sumu hiyo.

Familia yake ilifungua kesi kuwashitaki wanausalama hao na hii inakuwa ni fidia kubwa zaidi kuwahi kulipwa familia ya marehemu ndani ya Colorado.

Kwa upande wake, mama mzazi wa McClain, Sheneen, amewashukuru waliomuunga mkono katika kesi hiyo, pia akisema kifo cha mwanawe huyo kitaleta mapinduzi makubwa.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments