Fei Toto, Mayele Wala Kiapo Kuifunga Namungo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 
Yanga leo watakuwa ugenini mkoani Lindi kumenyana na Namungo katika mchezo wa mzunguko wa sita wa ligi kuu ambapo mchezo huo utapigwa katika Uwanja wa Ilulu uliopo mkoani humo.


Katika ligi hiyo Yanga kwa sasa ndio vinara wa ligi wakiwa wamejikusanyia jumla ya alama 15 mara baada ya kufanikiwa kushinda michezo yake yote waliyocheza.


Akizungumza na Championi Jumamosi, kiungo wa timu hiyo, Feisal Salum ‘Fei Toto’ alisema kuwa malengo yao ni kuendeleza ushindi ambao wameupata katika michezo mitano iliyopita huku mshambuliaji Fiston Mayele yeye akisema kuwa kila mchezo kwao wanauchukulia kama fainali, hivyo watapambana kwa ajili ya kuondoka na ushindi.


“Tumeshinda michezo yetu mitano ya mwanzo wa ligi, hakuna ambaye anasema sasa inatosha mpaka pale tutakapoona kuwa tumetimiza malengo yetu.


“Kila mtu anafahamu kuwa Yanga msimu huu tunahitaji ubingwa, hivyo hatutakubali kuona tunapoteza mchezo wowote uliopo mbele yetu,” alisema Feisal.


Mayele alisema: “Kila mchezo kwetu tunauona kama ni fainali, hakuna ambaye hafahamu timu huwa zinacheza vipi katika mechi za fainali, huwa zinapambana sana, basi na sisi tupo hivyo yote ni kuhakikisha tunatwaa ubingwa msimu huu.

STORI NA MARCO MZUMBE
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad