Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Real Madrid Waona Isiwe Tabu Waamua Kuachana na Mbappe
UONGOZI wa Real Madrid umeona ni bora kuachana na mpango wa kumchukua mshambuliaji wa PSG na timu ya Taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappe, kupitia usajili wa Januari, mwakani.

Uamuzi wao huo umekuja baada ya kukubaliana wasubiri mwishoni mwa msimu huu kwa kuwa Mbappe atakuwa mchezaji huru.

Kwa kuwa Mbappe atakuwa na mkataba kufikia Januari, Madrid watalazimika kulipa kiasi kikubwa cha fedha, ambacho hakitakuwepo majira ya kiangazi kwa sababu atakuwa amemaliza mkataba wake na PSG.

Madrid wamejaribu mara kadhaa kuinasa saini ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 na miezi michache iliyopita Rais wa klabu hiyo ya La Liga, Florentino Perez, alisema atamchukua ifikapo Januari.

 Download Our Udaku Special APP Kutoka Google Play Store Kwa Kutumia Link Hii Hapa>>>

Post a Comment

0 Comments