Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Mwanamke Mwingine Akutwa Amekufa Arusha

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

 


Arusha. Mwanamke mwingine mkazi wa Njiro jijini Arusha, Janerose Dewasi (66) amekutwa amefariki dunia nyumbani kwake baada ya kupigwa na kitu chenye ncha kali.

Tukio hilo limetokea siku chache baada ya mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite, Ruth Mmassy anayedaiwa kuuawa na mtoto wake

Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Justine Masejo amethibitisha kutokea tukio hilo leo Jumatano Desemba 29, 2021 na kueleza kuwa wanamsaka mfanyakazi wa ndani ambaye  alikuwa anaishi na marehemu huyo.

Kamanda Masejo amesema mwili wa mwanamke huyo aliyekuwa anaishi na mfanyakazi wa ndani kwenye nyumba yake eneo la block D amekutwa amepigwa na kitu chenye ncha kali kwenye paji la uso huku akibainisha kuwa Jeshi la Polisi linamsaka mfanyakazi wa ndani ambaye anadaiwa kutoroka muda mfupi kabla ya kugundulika tukio hilo.

"Uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu alikuwa anaishi na mtumishi wa kazi za ndani ambaye alianza kazi wiki moja iliyopita" amesema

Amesema kuwa mfanbyakazi huyo alitoweka muda mfupi kabla ya kugundulika tukio hilo.

Kamanda amesema Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wenye nyumba kuwa makini na wafanyakazi wa ndani wanaowapa kazi kwa kujua historia zao.

Mmoja wa majirani wa nyumba hiyo, Mary Muchi amesema mtuhumiwa huyo huyo alikuwa hajulikani sana mtaani kwani ameanza kazi muda si mrefu.

"Hatujui lolote huyo kijana anatajwa, alikuwa akiimsaidia huyu mama kazi zao na leo tumeshangaa kupata taarifa za kifo cha mama huyu"amesema.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments