DC Ilala aingilia kati sakata la nyumba iliyabomolewa kisa deni la Sh300, 000

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Selina Chacha, mkazi wa Kitunda Nyantira jijini Dar es Salaam akilia mbele ya nyumba yake iliyobomolewa Januari 6, 2021 kwa kile kinachodaiwa kuwa nyumba hiyo iliuzwa kwa njia ya mnada bila yeye kujua. Picha na Aurea Simtowe
Dar es Salaam. Siku chache baada ya gazeti la Mwananchi kuripoti juu ya familia ya Nyahure Range kuvunjiwa nyumba kwa kile kinachodaiwa kuwa nyumba hiyo imeshauzwa, Mkuu wa Wilaya ya Ilala (DC), Ng'wilabuzu Ludigija ameiita familia hiyo ofisini kwake pamoja na waliohusika na kuvunja nyumba hiyo.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Januari 12, 2021 mmiliki wa nyumba hiyo, Nyahure Range amesema wameagizwa kufika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala kesho kwa ajili ya kusikilizwa.

Nyahure amesema “Mkuu wa wilaya katutaka tukutane ofisini kwake kesho tukiwa na watu wa Kitunda Saccos na Broker (dalali),” amesema Nyahure.

Tukio la nyumba kuvinjwa lilifanyika Januari 6, 2022 ikiwa ni siku chache kabla ya kutolewa kwa hukumu ya Rufaa iliyokatwa na Selina Chacha ambaye ni mke wa Range kutolewa Februari 15 mwaka huu.


 
Nyumba ilivunjwa kwa kile kilichodaiwa kuwa familia hiyo ilikuwa ikidaiwa Sh300, 000 na Kitunda Saccos huku taarifa ya Kabango General Business ikionyesha kuwa familia hiyo ilitakiwa kuacha nyumba hiyo na mali zao kukamatwa ili kufidia Sh9.9 milioni.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad