TANZIA: Balozi Nchimbi afiwa na baba yake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Dar es Salaam. Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Dk Emmanuel Nchimbi amefiwa na baba yake mzazi, John Nchimbi usiku wa kuamkia leo Jumapili Januari 23, 2022 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) alikokuwa akipatiwa matibabu.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo baada ya kufika nyumbani kwa marehemu Tabata Relini, John Nchimbi ambaye ni mtoto wa marehemu amesema baba yake amefariki kwa ugonjwa wa moyo uliokuwa ukimsumbua kwa muda mrefu.

“Mzee wetu alikuwa na matatizo ya moyo lakini siku tatu zilizopita hali yake ilibadilika na alichukuliwa kwenda kwenye vipimo hospitali ya TMJ, baada ya kupata vipimo kesho yake hali yake iliendelea kuwa mbaya kwa hiyo tuliamua kumuamishia JKCI kwa ajili ya vipimo zaidi.

“Na katika vipimo walibaini mishipa yake ya upande wa kulia na kushoto inayotoka kwenye moyo imeziba ambayo huwezi kuzibua kwa kutumia waya na ilitakiwa afanyiwe upasuaji mkubwa wa moyo ili kutengeneza njia nyingine na mingine kuibadilisha. Wakiwa kwenye mchakato wa kufanya hivyo ilipofika saa nane usiku wa kuamkia leo baba akafariki,”amesema.


John Nchimbi ambaye ni mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya kiteto amesema baada ya taarifa hiyo maandalizi yanaendelea na Januari 25,2022 wanatarajia kuupumzisha mwili kwenye makaburi ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam.

“Mzee wetu alikuwa Kamshina wa Jeshi la Polisi, alikuwa kwenye siasa kwa hiyo kutakuwa na miongozo ya kiserikali kwa sababu alilitumikia taifa kwa mara ya mwisho akiwa kama Kamanda wa Polisi wa Mtwara kabla ya kustaafu mwaka 1996,”amesema

Nchimbi amesema baba yake amefariki akiwa na miaka 77  akiacha  mjane na watoto saba
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad