Wachezaji Maarufu Wa Mpira Tanzania Ni Nani Aliye Waroga?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Wakuu, Tumekuwa Tukiona Wasanii Wa Tanzania Wakisign Deals na Kampuni mbalimbali ya Kuwa Mabalozi wa kampuni husika na Kujiingizia Kipato kikubwa kwenye Mifuko Yako, Hii inatokea hata kwa Wale wasanii ambao wanavuma na Nyimbo 2 au Tatu wamekuwa Wakilamba Baadhi Ya Deals Katika kampuni. Ipo kwa Wasanii wa Muziki, Comedy, Movies na Wengine hata wasiojulikana.


Lakini Hii imekuwa Tofauti sana kwa WACHEZAJI MAARUFU WA MPIRA WA MIGUU TANZANIA. Sijawahi Sikia Mchezaji Wa mpira yeyote Tanzania akisign Deals Na Kampuni yoyote ile ambayo itamsaidia yeye kujipatia kipato chake nje ya Kazi ya Mpira na Kuendesha Maisha Yake ya Kila siku. Unaweza kukuta mchezaji wa Mpira ni mzuri sana Na Anafuatiliwa kila siku na Kusemwa kila leo Lakini Hakuna Deal Yoyote anayo sign itakayo msaidia Kujiingizia Kipato. Hii imekuwa ni Ngumu kwa wao hata Kufungua Biashara ambazo zitamuingizia Pesa Kupitia Jina na Kipaje chake Nje ya Kutegemea Mshahara.


Mara kadhaa nimeona Wachezaji mpira maarufu wa Tanzania, Wakitumiwa Sura zao Kwenye Matangazo ya GSM na MO kufanya Promotion ya Bidhaa mbalimbali Lakini sina hakika Kama Wananufaika na Vipaji vyao na Majina Yao katika hizo kampuni. Ni wazi kuwa hizi kampuni ambazo zina dhamini Vilabu Vya Mpira Tanzania Vimekuwa Vikiwatumia wachezaji hawa kujitangaza bila Mchezaji kulipwa na Kunufaika na Matumizi ya Jina lake, Sura Yake na Kipaji chake kujipatia Pesa Kitu Ambacho ni Tofauti na wasanii na Wachezaji wa Mpira Wa nje ya Tanzania.


Ieleweke kuwa, Club Ikimsajiri mchezaji Inamsajiri kwa Lengo la Matumizi ya Club uwanjani na Sio kwa Lengo la Kutangaza Bidhaa za Kampuni Inayodhamini Hiyo club. Kwa Wachezaji wetu wa Tanzania Shida ni Nini? Je shida ni management ya Mchezaji kutokuelewa Umuhimu wa Kipaji chake na Jina Lake? Au Ni unyongwaji unaofanywa na haya Makampuni?


Tumeona Wachezaji wa Ulaya, Wasanii wa Tanzania Hata wasemaji wa hivi vilabu vyetu wakisign Deals na kampuni mbalimbali kutangaza bidhaa zao na kufanya wanufaike na Umaarufu wao, lakini hii imekuwa Tofauti kwa Wachezaji wetu. Tumeona Wachezaji na Wasanii wakifungua biashara kubwa na kuzikuza Kupitia Majina Yao na Umaarufu wao kujipatia Kipato na kuweza kuishi vizuri lakini kwa Watu maarufu wanaocheza mpira Tanzania Hii imekuwa Tofauti sana.


Tatizo liko Wapi kwa Wachezaji wa Mpira Tanzania? Wanaelewa Dhamani Yao?


Hebu angalia Mchezaji kama Chama Alivyokuwa maarufu Tanzania, Mchezaji kama Morrison, Mayele, Aucho, Wawa, Manura, Kagere, Mkude, Bocco, Na wengine Wengi, Hawana Biashara zozote wanazo zifanya, Hawana Mikataba na kampuni zozote kwaajiri ya Ubalozi na Tegemeo lao kubwa ni Mshahara wa Mwisho wa Mwezi. Ndio maana Wakiacha kucheza Mpira wanakosa hata pesa Ya Nyumba au Dawa.


Je Wachezaji Maarufu Wa Mpira Ni Nani Aliye waroga?


Management zao? Au ni wao kushindwa Kujitambua? Inaumiza Sanaa.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad