Jinsi Kumshikia Mtu zamu ya Kuuza Duka Kulivyosababisha BINTI Huyu Akawa Mke wa Cristiano Ronaldo - Part 2

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




GEORGINA RODRIGUEZ UDHURU ILIMPA RONALDO (PART 2)

Wakati wamekutana tena pale kwenye maonesho ya Gucci, Ronaldo akiwa na Kaka yake akamuita Gio na kusalimiana nae kisha akamwambia kama wanaweza kutoka dinner

Gio anasema usiku ule walikuwa na party ya pamoja wafanyakazi wa Gucci, hivyo ikabidi awakatae wenzake na kukubali kwenda kwa Ronaldo kula chakula cha jioni

Wakati wapo kwenye gari Gio anasema mikono yao iligusana kwa bahati mbaya tu ila kwa namna hisia zilivyo kati yao wakashindwa kujizuia akakutana wameshika rasmi mikono

Binti anasema walipofika nyumbani kwa Ronaldo mitaa ya FINCA, kwanza alishangazwa na ukubwa wa nyumba lakini pia namna Ronaldo aliagiza kiandaliwe chakula kizuri sana ambacho yeye alikipenda

Ronaldo hakuwahi kuonekana ana haraka Wala papara, hakuwahi kutaka kutumia jina lake kumnasa Binti huyo bali vitendo tu, baada ya kula Ronaldo alimrejesha nyumbani kwake

Wakati mapenzi yao yanaendelea kunoga, Ronaldo alisafiri kuelekea timu ya taifa, Gio anasema alimmiss sana Ronaldo na hakumtafuta kwa muda kidogo, alikuwa anaogopa kumuanza Ronaldo hivyo muda wote alikuwa anasubiri tu simu

Baada ya siku kama tano kupita wakati Ronaldo karejea Madrid, akakutana na simu ya CR7 alimuuliza ni wapi alipo na Binti kwa aibu aibu akamwambia yupo kwake, CR7 akamwambia anamfuata watoke

Usiku ule ndipo Gio akaondoka na baadhi ya nguo zake kwenda kwa Ronaldo, alilala kwa Gwiji siku ile😃 Mnyama anasema waliishi kwenye dunia yao usiku ule

Gio kutokana na 'ushamba' asubuhi aliamka na kuanza kuzunguka mjengo wa CR7 alipotea mara nyingi kutokana na ukubwa wa jengo


Wakati tayari amewahi kwenda kwa Ronaldo kama mara mbili ila bado hakuwa amemzoea hivyo kutokana tu na ukubwa wa Ronaldo Ijapo Gwiji alikuwa simpo tu kwa Binti 

Ronaldo anasema hakutegemea kama angedumu eneo Hilo lakini kwa kadri muda ulivyokuwa unasonga akaanza kumuelewa zaidi (Gwiji alikuwa kama anataka tu kupita njia)😃

Siku moja baada ya mechi ya Real Madrid na Athletic Bilbao, Binti akiwa amemaliza kuitazama hiyo mechi, nafsi yake ikawa inasubiri tu aitwe na Ronaldo, kipindi hicho alikuwa anaishi alipopanga, floor ya chini kati mwa Madrid

Ghafla Gio anakutana na text ya Gwiji, Mambo, unaendeleaje? Upo free? Texts mbili hizo majira ya saa nne usiku! Binti anasema alikuwa kashamaliza Kila kitu, hivyo akajibu nipo free ila nilitaka kulala sasa hivi (si unajua Dada zetu😃)

Gwiji akauliza tu naweza kukupitia tutoke? Gio unadhani angechelewa wakati alikuwa anasubiri hicho tu😃 (Wanangu Kuna cha kujifunza hapa, Mwanamke anapaswa kubembeleza usiwe machumachuma)

Kwakuwa kesho ilikuwa siku ya kazi hivyo Gio kama kawaida yake, akapack nguo kwenye kibegi chake Ili akilala kwa Gwiji asubuhi adamke kazini (kumbuka alikuwa Bado hajaacha kazi)

Bernabeu na alipokuwa anaishi Binti hapakuwa mbali, baada ya dakika chache Bugatti la Gwiji linapiga honi, Binti anatoka wanaondoka zao, taratibu akaanza kumzoea Mnyama licha ya kuwa tayari walishaanza mambo flani😃

Kwakuwa Binti alikuwa Bado Mfanyakazi wa Gucci hivyo CR7 alikuwa anaenda kumsubiri nje ya duka mpaka saa 4 usiku Ili waondoke wote (mahaba niuwe, sio ile mpe boda simu 😃)

Ikafika wakati Ronaldo alimwambia Binti haoni sababu ya kuendelea kujificha hivyo atakuwa anakuja kumchukua kazini na ndinga zake Kali kama Bugatti Veyron au Lamborghini, Gwiji Mtanashati Bwana😃

Sasa Kuna sehemu nilisema Bado Binti haijui vyema nyumba ya Ronaldo kutokana na ukubwa, siku moja....


Niliishia kuwa Gio bado alikuwa haifahamu vyema nyumba ya Ronaldo kutokana na ukubwa wake na mara nyingi alikuwa anapotea (si unajua katika hali ya Binti kujionesha pia kwa wadada wa kazi 😃)

Ronaldo anasema kuwa lengo lake halikuwa kukaa sana kwa Binti ila baadae akatokea kumpenda ikichagizwa pia na maisha magumu sana ambayo Binti amepitia, Gwiji akaona atende wema pia na akapenda mazima

Jumlisha pia Dada zake, Mama, Kaka na Washikaji zake walishampitisha kuwa hana tatizo (bila kusahau na wakina 'Aristote wa Ulaya) nao walisema Binti anafaa, maana Gwiji haamui peke yake, si unajua Gwiji ni last born huyu kwao

Wakati media zinahaha wakina @mwijaku_01 wa Ulaya Wakitaka kujua Ronaldo anatoka na nani, Bado ilikuwa ngumu hata Wafanyakazi wenzake Binti waliona tu Bugatti inapark nje ya duka, Binti anapanda wanasepa,  Ronaldo alikuwa hatoki nje

Ronaldo anasema katika vitu ambavyo alivipenda ni kitendo cha Binti kumuelewa mapema sana Gwiji kipi anapenda na kipi hapendi, moja wapo ni kuwa Gio alifahamu Ronaldo usiku wa kuamkia mechi huwa hachezi mechi (tumeelewana) 

Gio pia aligundua Gwiji usiku wa kuamkia mechi huwa hatoki out yoyote, pia analala mapema sana, hivyo hata siku akienda nyumbani kwa Gwiji akawa anafanya vitu vya msingi tu, baada ya mechi ndipo atapewa mechi yake 😃

Binti alijitahidi sana kuendana na maisha ya Ronaldo ila muda wote anamsifia Gwiji kuwa anajua kujali mno, ikiwemo kuogeshwa, kununuliwa vitu vizuri vya gharama kama zawadi 

Lakini bado Ronaldo alijitahidi kujitofautisha yule Staa wa dunia na yule Mpenzi wa Gio, Binti anasema Gwiji hana matumizi mengi ya simu zaidi ya kupumzika, mazoezi na kupumzika nae, wakiwa free

Kiangazi cha 2016 Binti alimuomba Ronaldo ampeleke Disneyland Paris, Ufaransa, Jiji la maraha hilo, sasa kimbembe ni kuwa........


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad