Kocha Pablo "Nitawashangaza Msimu Huu"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



KOCHA Mkuu wa Simba SC, Pablo Franco, amesema atawashangaza wengi msimu huu kwani wana imani ya kutwaa makombe yote ambayo wanayatetea licha ya kuwa katika mwendo wa kusuasua ndani ya Ligi Kuu Bara.


Simba inatetea taji la ligi na kwenye msimamo ipo nafasi ya pili ikikusanya pointi 28. Pia inatetea taji la Kombe la
Shirikisho la Azam Sports ikiwa tayari imetinga hatua ya 16 bora.

Kutokana na mwendo wao huo, wengi wamekuwa wakiitoa Simba kwenye mbio za ubingwa, huku Yanga inayoongoza msimamo kwa sasa ikiwa na pointi 35 kabla ya mechi ya jana, ikipewa nafasi kubwa zaidi ya kuwa mabingwa.


Akizungumza na Spoti Xtra, Pablo alisema: “Tunakwenda kwa mwendo huu ambao haujawa mzuri, ni kweli kwani
mpira sio hisabati, ni namna ambavyo tunafanya uwanjani, hakuna tatizo, malengo yetu ni
kuchukua ubingwa wa ligi na Kombe la Shirikisho.

“Hili niliweka wazi tangu mwanzo, ligi bado inaendelea na Kombe la Shirikisho tumefika hatua nzuri, kikubwa ni kuwa na subira na wachezaji ninaamini watafanya vizuri na kuwashangaza.” Leo Jumapili, Simba inatarajiwa kucheza dhidi ya Mbeya Kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar kuanzia saa 1:00 usiku.


Hii itakuwa ni mara kwanza kwa timu hizi kukutana kwenye ligi kuu ambapo Simba inashika nafasi ya pili kwenye
msimamo huku Mbeya Kwanza inayoshiriki ligi kuu kwa mara ya kwanza, ikiwa ya 12 kabla ya
mechi za jana.


Pablo leo Jumapili, anatarajiwa kumaliza adhabu yake ya kukosa mechi tatu baada ya kufungiwa hivi karibuni ambapo tayari amezikosa mbili dhidi ya Dar City na Prisons
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad