Msanii Wa Muziki Wa Bongo Fleva Lulu Diva Atoa Neno Msiba wa Mama yake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Msanii Wa Muziki Wa Bongo Fleva @luludiva ametoa Shukrani zake za dhati kwa wote waliokuwa na katika msiba Wa mama yake mzazi.

Kupitia ukurasa wake rasmi Wa Instagram ameandika✍️✍️✍️

"Leo ni siku ya Pili Sasa Tangu KUMALIZA arobaini ya msiba wa Mama yangu nikaona haitakuwa busara kama sitachukua nafasi hii kutoa neno la shukurani".

"Kutoka moyoni mwangu napenda kutoa SHUKRANI ZANGU ZA DHATI kwa wote waliokuwa na mimi katika kipindi hiki kigumu, upendo mlionionesha ni mkubwa mnoo, nikiri SIKUUTEGEMEA,"

"Na niseme tu Namshukuru MUNGU sana kwa ajili yenu, mmenifariji sana!!!! Hii ni kwa kila mmoja aliejitoa juu yangu kwa hali na mali, Wasanii wenzangu, Viongozi mbalimbali, Vyombo vya habari, Wadau tofauti, Mashabiki zangu, ndugu, jamaa marafiki na Watanzania wote walioguswa kwa ujumla, iwe kwa kuja kuniona, kwa kunipigia simu, kwa kusafiri na mimi, kwa post za faraja na kwa namna yoyote ile, kutoka moyoni mwangu kabisa nawashukuru sana sana WOTE na NINATHAMINI 🙏"

"Lakini pia kwa MAKAMPUNI YOTE ninayofanya nayo kazi, nawashukuru sana kwa uvumilivu wenu kwangu kwa muda wote wa maombolezo,"

"Najua nina majukumu ya kikazi na vitu vingi hata vya kupost kimikataba, lakini mlinipa muda na kuacha nimourn, niseme nini juu yenu zaidi ya kuwashukuru kwa UTU mlionionesha".

"Nikiwa kama mtoto pekee kwa Mama yangu Ukaribu wetu haukuwa wa kawaida, nakiri NIMEONDOKEWA!! kwangu hili ni PIGO zito,"

" Na kiubinaadamu maumivu yake hayaelezeki, lakini pamoja na yote MUNGU ametuagiza tushukuru kwa nyakati zote hivyo namshukuru kwa kila jambo na sina complain yoyote juu ya kazi yake, yeye ndio alietoa na yeye ndio alietwaa!!"

"Kuendelea kukaa ndani sio kitu ambacho hata Mamaangu angependa, maisha lazima yaendelee ukizingatia nina kazi na watu wengi ambao wamenipa muda wa kutosha na kuna mengi binafsi yako mbele yangu kwasasa, Mama hayupo lakini MUNGU yupo!! Yeye aliemchukua ndio atajua namna gani atanifariji".

"Niwashukuru tena nyote kwa mara nyingine kwa upendo na ushirikiano wenu mkubwa!! MUNGU awabariki sana kwa namna mlivyonishika, na akawaguse kama mlivyonigusa, ASANTENI SANA".

"Inalillahi Wainailaihi Rajiun
Pumzika kwa amani kipenzi changu
Forever in my Heart MAMA 🌹".
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad