Kapombe Apewa Tuzo ya Mchezaji Bora Februari

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Beki wa kulia wa klabu ya Simba SC Shomari Kapombe, amekabidhiwa tuzo yake ya mchezaji bora wa mwezi Februari wa mashabiki wa klabu hiyo (Fans Player of the Month), ameshinda kiasi cha shilingi milioni 2 .

Kapombe ameshinda tuzo hiyo baada ya kuwapiku wachezaji wenzake aliokuwa akishindana nao kuwania tuzo hiyo ambao ni winga Peter Banda na mlinzi wa kati Henock Inonga ambao aliingia nao fainali katika kinyang’anyiro hicho. Katika mwezi Februari Kapombe alicheza mechi 4 ambapo alifunga bao 1 na alihusika kwenye kutengeneza mabao mengine 2.


Baada ya kushinda tuzo hiyo beki huyo wa kimataifa wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars amesema tuzo hiyo ni muhimu kwao kama wachezaji kwasbabau inawaongezea hali yakupambana zaidi,


“Kwanza niwashukuru Emirate kwa kudhamini tuzo hii, inaongeza morali kwetu kama wachezaji. Pia niwashukuru wachezaji wenzangu kwa ushiriakiano mkubwa walionipa. Kwangu hii ni changamoto ambayo inanifanya niendelee kujituma kwa ajili ya kuisaidia timu kufanya vizuri na ndio lengo la kila mchezaji wa Simba.” amesema Kapombe.


Wakati mashabiki wa kikosi hicho cha mabingwa wa Tanzania bara wakiendelea kuwapigia kura wachezaji wao wanaofanya vizuri kila mwezi na kushinda tuzo hizo, lakini klabu ya Simba bado haijashinda tuzo ya mchezaji bora wala kocha bora wa mwezi kwenye tuzo za Ligi Kuu soka Tanzania bara zinazotolewa na kamati ya tuzo yaLigi Kuu.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad