Putin Kuburuzwa Mahakama ya kimataifa (ICC)

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



MAHAKAMA ya Kimataifa ya Uhalifu ICC inatarajia kuanza uchunguzi kuhusu uwezekano wa uhalifu wa kivita nchini Ukraine hali ambayo inatafsiriwa kumweka matatani Rais wa Urusi, Vladimir Putin. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hatua hiyo imekuja baada ya jana tarehe 1 Machi, 2022 Mwendesha mashtaka mkuu wa ICC, Karim Khan kusema kuwa mahakama hiyo itaanzisha uchunguzi kuhusu uwezekano wa uhalifu wa kivita unaofanywa na Urusi nchini Ukraine.

Katika taarifa, Khan amesema maamuzi ya uchunguzi kuhusiana na hali nchini Ukraine haraka yataanza haraka iwezekanavyo.

Khan amesema baada ya kupitia uchunguzi wa awali wa hali hiyo, ameridhika kwamba kuna sababu za kimsingi za kuamini kwamba madai yote ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu vimefanyika nchini Ukraine katika matukio kabla ya uvamizi wa Urusi.


Khan ameongeza kuwa kwa kuzingatia kupanuka kwa mzozo huo katika siku za hivi karibuni, ni nia yake kwamba uchunguzi huo pia utajumuisha madai yoyote mapya ya uhalifu yaliyo chini ya mamlaka ya ofisi yake ambayo yatafanywa na pande yoyote katika mzozo huo katika eneo lolote la Ukraine.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad