Ticker

6/recent/ticker-posts

Haji Manara "Sio Kila Vita Inayokuja Mbele Yako lazima Upigane Nayo"

 Habari Kama Hizi Zinapatikana UDAKU SPECIAL App, Download HAPA Bure: Link here>>>Kila siku kuna watu mahali watakuwa wanatamani Anguko lako.

Sio kwa sababu umewafanyia Kitu Kibaya, la hasha - Wakati mwingine hata unapowatendea mema.

Kuna watu wanachukia wewe kuwa na nafasi uliyonayo,na cha kushangaza hata ukiwa haupo hapo wao hawawezi kuipata hyo nafasi .

Kuna watu wanachukia kwa sababu ya vitu ulivyonavyo na hata hawataki kujiuliza umevipataje.hufikiria umevipata kwa fluk bila kuangalia jitihada zako za namna unavyopigana kujikwamua katika umasikini

Kuna watu watakusema vibaya kwa Maneno ya uongo ili wakuharibie sifa zako na kuchafua jina lako hata wakati wewe hauna ugomvi nao. na wengine huwajui na hata hamfahamiani hata chembe.

Kuna watu watakuja kuwa karibu na wewe ili tu wakufahamu vizuri na kutumia kila udhaifu watakaoupata kukushusha chini.wanaweza kukusingizia uovu mkubwa usiojua chanzo chake ni nini.

Katika makundi haya Unatakiwa kuwa makini.lazma uwe na machaguo sahihi ya aina ya watu wanaostahili kukukurubia.

Kuna ambao wanastahili Muda wako na Nguvu zako za kupambana nao lakini wengi HAWASTAHILI kabisa Muda na Nguvu zako...

...kwa sababu wamekuja kama “VISION DISTRACTORS”(Watu ambao wanafanya Mambo ili wakutoe kwenye mstari).

Kumbuka sio KILA VITA INAYOKUJA MBELE YAKO unatakiwa KUPAMBANA NAYO.

Sio kila mtu unatakiwa KUMJIBU. Wengi wao ni kuwapuuza na hapa usikubali kujibu tuhuma za hovyo hovyo zinazotengezwa kwako toka huku mitandaoni,,kwa nafasi yako kubali kusingiziwa hata machafu coz huku hatujuani tunasomana na kuhukumiana vile mtu anavyojisikia

Wengine unapoanza kuwajibu tu ndio UMEWAPA USHINDI.

Amua kila siku kuwa “FOCUSED” na kile unchofanya na USIKATISHWE tamaa na watu wa namna hii.

Ramadhani Kareem

Tupo live now kuanzia Saa saba na Robo Kwenye MANARA TV (@hajimanaratv) kukuletea Press yetu.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

________________________________

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments