Wasaouth ni Kawaida yao Kulalamika Kila Jambo...Pirates Watuonyeshe Hizo Hujuma Walizodai Kufanyiwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Anaandika @salehjembefacts, Niwaeleze jambo,
Ukimsikiliza kocha huyu wa Orlando Pirates, unaweza kusikitika sana na leo unaona ndiye amekuwa gumzo kwa kuwa sisi Watanzania ni wepesi kuamini ya kuambiwa kuliko tunayoona.
Kawaida ya watu wa Afrika Kusini ni kulalamika kila jambo hata kama hawa uthibitisho. MFANO, Kocha huyu analalamikia VAR haikufanya kazi, tena anawalalamikia Simba na sisi tunaamini, JABU!
Tunajua sote Caf ndio wahusika ndio wenye mashindano yao, vipi awalalamikie Simba? Nani ana uthibitishi VAR haikufanya kazi? If hakuna sasa kwa nini tunaamini na macho yanatuonyesha mwamuzi alifanya mawasiliano na watu wa VAR na unaona aliwaambia wachezaji wa Orlando kwa ishara kuwa watu wa VAR ndio wamethibitisha baada ya kupata sekunde kadhaa za kuwasiliana nao.

Achana na hiyo, kocha anasema hawajatengewa haki au walifanyiwa vitendo visivyo sijui kuanzia hotelini.

Simba wanahusikaje na hoteli waliyotafuta na kufikia wao? Kama ni barabarani ni vitendo vipi, mbona hawasemi?

Ukiwa makini utagundua ni mwendelezo wa propaganda ya kipuuzi kabisa ambayo inatokana na tabia za watu wa Afrika Kusini kuamini wao ni kila kitu na kulalamikaaaa ndio maisha.

Angalia, kocha analalamika lakini hana hata mfano mmoja wa matukio waliyifanyiwa.


Mwambieni kocha aache siasa kwenye mpira, suala la WE ARE AFRICAN wala lisiwe kisingizio cha kila kitu wanaposhindwa na mumkumbushe…


@ Simba haina mwamuzi
@ Simba haina uwezo wa kujipa au kuwanyima penalty, awasiliane na Caf
@ Simba haikuwapangia hoteli, haina uwezo wa kwenda kuwanyanyasa hotelini

Mwambieni Simba wameshinda mara Chungu mzima dhidi ya vigogo kama Al Ahly, Zamalek na wengine kibao.

Nawakumbusha, hawa Orlando walitengeneza propaganda kuwa Simba wanahonga waamuzi, wakasingizia moja ya gazeti lao kufanya mahojiano na Abdi Banda ambaye alipinga na kuniambia hakuwa amezungumza na mwandishi yoyote wa hapa au Afrika Kusini kwa muda mrefu.
Wamefungwa, zamu ya Simba kwenda kupambana na ikiwezekana itakuwa bora, ikishindikana ndio mpira lakini vizuri nawe jifunze, si kila KINACHOZUNGUMZWA KWA KIINGEREZA BASI KINA MASHIKO SANA.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad