Ticker

6/recent/ticker-posts

Hatimaye Diamond Platnumz Ataja Muda Atakao Nunua Ndege yake Binafsi


Baada ya kuweka wazi kuhusu kununua ndege yake binasfi (private jet) ndani ya mwaka huu, Staa wa muziki nchini na CEO wa record label ya WcB wasafi @diamondplatnumz sasa ameweka wazi kuhusu ndege hio kwa kusema ndege hiyo huenda ikatua nchini kabla ya mwezi Oktoba, kuelekea siku yake ya kuzaliwa.

Platnumz ambae kwa sasa yupo nchini ivory coast katika muendelezo wa ziara yake ya kuitangaza EP yake ya FOA, ameeleza hayo kwenye moja ya mahojiano yake akiwa nchini humo akisema kuwa analazimika kununua ndege hiyo ili kupunguza matumizi makubwa kwenye safari zake.

"Inanilazimu ninunue ndege yangu binafsi kwa sababu watu ambao nasafiri nao kwenda sehemu mbalimbali ni wengi sana kwahiyo ni gharama kulipia. Kununua ndege yangu binafsi sio suala la anasa bali ni kupunguza matumizi makubwa kwangu.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments