Ticker

6/recent/ticker-posts

Azam FC yaanza kutambulisha vifaa, tajiri aahidi mazitoKlabu ya Azam FC imekamilisha Usajili wa Kiungo Mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast, Kipre Junior Kwa mkataba wa miaka mitatu.


Staa huyo ambaye jina lake kamili ni Kipre Junior Zunon Tiagouri Emmanuel, amenunuliwa na Azam FC kutokea timu ya Sol FC ya kwao,Na pichani akisaini mkataba mbele ya mmiliki wa timu, Yusuf Bakhresa (@yusufbakhresa) na Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin (@abdulkarim.amin).


Nyota huyo aliyekuwemo kwenye kikosi bora cha msimu huu wa Ligi Kuu ya Ivory Coast (Ligue 1), amewahi kusajiliwa na miamba ya Ufaransa, Strarsbourg msimu wa 2017-2018.


Kiungo huyo mshambuliaji, 22, mwenye kipaji cha hali ya juu pia aliwahi kuwatumikia vigogo wa Ivory Coast, Asec Mimosas, 2018-2020.


Ubora wake ulimfanya pia kuchezea timu za Taifa za vijana za Ivory Coast U-15 na U-17, pamoja na kikosi cha wachezaji wa ndani (CHAN) 2020.


Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments