Ticker

6/recent/ticker-posts

Bondia Tyson Afunguka "Siku Yanga ya Kufa Imekaribia"


 “We’re all gonna die one day, of course,” Says Tyson, “Then, when I look in the mirror, I see those little spots on my face, I say, ‘Wow. That’s my expiration date is coming close, really soon.’” Hayo ni maneno ya bondia mkongwe Mike Tyson (56), ambapo ni maneno ya kushtua na kushangaza kwa kudai siku yake ya kufa imekaribia.


"Sote tutakufa siku moja bila shaka. Kila ninapojitazama kwenye kioo naona madoa madogo usoni mwangu, hiyo ina maana siku yangu ya mwisho wa kuishi inakaribia, iko karibu sana'." - Tyson ameeleza hayo kupitia Podcast yake iitwayo "Hotboxin", ambapo alikuwa na mtaalamu wa tiba ya afya ya akili, pamoja na uraibu wa madawa, Sean McFarland.


Ikumbukwe kuwa, hii sio mara ya kwanza kwa Tyson kukijadili kuhusu kifo chake cha baadae. Akiwa kwenye moja ya mkutano wake na walemavu wa akili huko Miami mwaka jana, aliweka wazi kuwa alishajaribu kunywa sumu ya chura wa jangwa la Sonoran kwa madhumuni ya kujitoa uhai wake.


Aidha, akiendelea kuzungumza kwenye podcast yake, pia amelaumu kwamba akiyaangalia maisha yake na wingi wa pesa alizonazo hazijawahi kumfanya aridhike na maisha.


“Money don’t mean s*** to me,” Tyson said. “I always tell people, they think money’s gonna make them happy..... "Pesa haimaanishi chochote kwangu, siku zote mimi huwaambia watu wanafikiria pesa itawafurahisha".


✍️: @omaryramsey


Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments