Ticker

6/recent/ticker-posts

Daktari akamatwa kwa kumbaka mjamzito

 


Daktari wa ganzi, Giovanni Quintella Bezerra anashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini Brazil baada ya kushtakiwa kwa kumbaka mgonjwa aliyelazwa wakati wa upasuaji katika Hospitali ya Wanawake ya Heloneida Studart ya Rio de Janeiro.


Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi nchini humo, Quintella alinaswa na ujumbe wa usaidizi wa Wanawake wa jiji hilo, baada ya uhalifu huo kurekodiwa kwenye video.


Maafisa wa polisi, wamesema walifika katika kituo hicho baada ya maafisa wa kitengo cha afya ambao walikuwa wakihofia utendaji wa daktari huyo wa ganzi na kumpiga picha wakati wa upasuaji.

Kitengo cha Habari kilichofanikiwa kupata kanda hiyo ya video wakati wa tukio la uhalifu, kimesema Quintella aliingiza uume wake katika kinywa cha mwanamke huyo akiwa usingizini kutokana na ganzi.


Polisi wamesema Quintella Bezerra anatuhumiwa kwa tukio la ubakaji dhidi ya mtu ambaye alikuwa hawezi kujitetea na kwamba atabiliwa na kifungo jela cha kati ya miaka 8 hadi 15 ikiwa atapatikana na hatia mbele ya Mahakama.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments