Dawa ya Mkongo yapigwa marufuku

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




BARAZA la Tiba Asili na Tiba Mbadala Tanzania, limepiga marufuku matumizi kwa binadamu dawa aina ya Hensha maarufu Mkongo, inayomilikiwa na kituo cha Nyasosi Traditional Clinic cha jijini Dar es Salaam na kuifutia usajili  dawa hiyo.

Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Prof. Hamisi Masanja Malebo, ametoa kauli hiyo leo Julai 27, 2022 mjini Morogoro wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Profesa Malebo alisema baraza katika uchunguzi wake lilibaini dawa iitwayo Hensha maarufu Mkongo, yenye usajili namba TZ17TM0027, ilikutwa imechanganywa na dawa ya kisasa ya nguvu za kiume iitwayo sildenafil, kwa jina maarufu la biashara Viagra ama Erecto.

Alisema kitendo hicho ni kinyume cha sheria na miongozo ya usajili wa dawa za tiba asili na mbadala.


 
Alisema kituo hicho kimetakiwa kuhakikisha kinaiondoa sokoni mara moja dawa hiyo, vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mmiliki.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad