Ticker

6/recent/ticker-posts

Kagere Amalizana na Simba Licha ya Kwenda Misri Hatakuwa Sehemu ya Kikosi Msimu UjaoINAELEZWA kuwa, straika wa Simba, Meddie Kagere, tayari amemalizana na uongozi wa klabu hiyo kwa baadhi ya mambo ambapo hatakuwa sehemu ya kikosi hicho msimu ujao, licha ya kusafiri na wenzake kwenda kambini Misri.

Kagere ni miongoni mwa wachezaji ambao Simba imepanga kuachana nao akiwa amebakiwa na mkataba wa mwaka mmoja, huku taratibu za kuuvunja mkataba huo zikiendelea.

Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka Simba, kililiambia Spoti Xtra kwamba: “Ni kweli Kagere ni miongoni mwa wachezaji ambao tunatarajia kumalizana nao na taratibu za kusitisha mkataba wake zinaendelea kwa makubaliano ya pande zote mbili.

“Licha ya kuungana na kikosi kwenye maandalizi ya msimu mpya, lakini hatakuwa sehemu ya kikosi kuelekea msimu ujao na tunatarajia kumuaga rasmi kikosi kikirejea kutoka nchini Misri.


 
“Ni miongoni mwa wachezaji ambao wametupa mafanikio makubwa ndani ya misimu minne aliyoitumikia Simba, hivyo tunatambua na kuuthamini mchango wake, tunamtakia kila la heri kwenye maisha mengine nje ya Simba.”

Stori: Musa Mateja na Hussein Msoleka

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments