Ticker

6/recent/ticker-posts

Mwanamke Adakwa Akimuuza Mtoto wake wa Siku Tano ili Apate Pesa za Kufanya Sajari ya Pua


Mdada huyo mwenye plasta(33) toka nchini Urusi amedakwa na vyombo vya sheria nchini humo kwa kumuuza mwanae wa kiume mwenye umri wa siku tano ili apate pesa za kwenda kufanya sajari kurekebisha pua yake hiyo ili azidi kuwa mzuri

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari na polisi wa Urusi, mrembo huyo baada ya kuzaa alimwambia rafiki yake hana nia ya kulea mtoto aliyemzaa, ambapo tayari alishazungumza na mwanamke na mwanaume(couple) waliokuwa washatoa pesa kiasi kumnunua mtoto husika ambapo jumla walikubaliana manunuzi hayo yawe £2900 ambazo sio chini ya milioni 7.9 za Tanzania

Couple iliyotaka kununua mtoto wakihojiwa na polisi wamesema, awali mdada huyo pichani aliwaambia hana kazi wala sehemu ya kuishi ndio anahitaji pesa

Baada ya kuwapa mtoto, mtoto husika hakuwa sawa kiafya hivyo hospitalini couple husika ikaulizwa cheti cha mtoto na hawakuwa nacho, waliporudi kwa huyo mama halisi wa mtoto kumuuliza kuhusu cheti cha mtoto akawataka wamalizie malipo yaliyobaki ndio awape cheti na safari hii akawaambia pesa hizo za kumuuza mwanae amepanga akafanye sajari ya pua ili kuongeza ubora wa urembo wake

Na kabla hawajamalizana kulipana malipo ndio wote watatu wakadakwa na vyombo vya sheria kwa biashara hiyo haramu ya kuuziana watu

Pichani mwenye plasta ndie aliyezaa na huyo mwingine ndie mnunuzi

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments