Ticker

6/recent/ticker-posts

Mahari ya Fahyma Yaongezeka Adai Uzuri Wake Umeongezeka Maradufu

 


FAHYMA au Fahyvanny; ni mwanamitindo na sosholaiti maarufu nchini Tanzania ambaye kwa mara nyingine ameibua gumzo kwenye mitandao ya kijamii baada ya kudai kwamba uzuri wake umeongezeka maradufu hivyo mahari imeongezeka kwa mwanaume yeyote mwenye mpango wa kumchumbia.


Fahyvanny ambaye wengi walimjua kutokana na kuchumbiana na msanii Rayvanny au Vanny Boy kiasi cha kutumia jina la msanii huyo na kuunda lake anasema kwamba uzuri wake kwa siku za hivi karibuni umezidi kunoga na bei ya mahari haitabaki palepale ilipokuwa kwani nayo lazima itii na kuongezeka vilevile.


 


Fahyma anasema; “Nyie nyie, naomba mahari iongezeke, siyo kwa uzuri huu…” Wafuasi wanaomfuatilia kwenye mtandao wa Instagram walionekana kumjibu makali mubashara huku wengi wakionekana kumsema kwamba hana uzuri wowote bali ni vipodozi tu ndivyo vimechangia kwa asilimia kubwa ya uzuri wake. “Mahari gani wakati hapo ukinyeshewa na mvua make-up inavuja na unakuwa mwingine kabisa, hapo bado sijaja kwenye filter za simu au basi tu,” mmoja alimsimanga.


 


Fahyma alikuwa na mahusiano ya muda mrefu na msanii Rayvanny mpaka mwaka wa 2019 ambapo alitangaza kuachana na msanii huyo baada ya kubarikiwa na mtoto mmoja.


Za chini ya zulia zilidai kwamba kuvunjika kwa mahusiano yao kulitokana na mwanadada aliyekuwa akicheza kwenye Video ya I Love You ya msanii huyo ila mwaandada huyo alikuja kuweka bayana kwamba hakuwa anachumbiana na Rayvanny.


Aidha, msanii huyo hajawahi kujitokeza hadharani kupinga wala kukiri madai hayo na sasa kuna taarifa kwamba Fahyma na Rayvanny wamerudiana.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments