Ticker

6/recent/ticker-posts

Matiko na Wenzake Kuangukia Mikononi Mwa KibatalaMahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetoa ruhusa ya Nusrati Hanje, Halima Mdee, Esther Matiko, Ester Bulaya, Jesca Kishoa na wenzao wawili kufika mahakamani na kuhojiwa na mawakili wa upande wa CHADEMA.

Mawakili wa upande wa CHADEMA wakiongozwa na Wakili Peter Kibatala, wakizungumza na vyombo vya habari amesema kuwa wamewataka Halima Mdee na wenzake kufika mahakami Agosti 26 wakati kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya maombi ya msingi kusikilizwa,  kwa mara ya kwanza ili wahojiwe kuhusu mchakato wa ubunge wao.

Haya ni maombi namba 36 ya mwaka 2022, yaliyofunguliwa na Halima Mdee na wenzake 18, dhidi ya Chadema Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Tume ya Taifa ya uchaguzi, yatasikilizwa mbele ya Jaji Cypiria Mkeha. 
Kesi hiyo kurejea maamuzi ya CHADEMA kuwavua unachama wao Halima Mdee na wenzake imeahirishwa hadi Agosti 26, itakapokuja mahakamani hapo kwa ajili ya kusikilizwa baada ya nyaraka za msingi kuwasilishwa mahakamani hapo

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments