Ticker

6/recent/ticker-posts

Mwanamuziki wa Nigeria Burna Boy Anaumizwa na Mapenzi, Awakosea Wanaocheza na Kufurahi Wimbo Wake Mpya wa Last Last"


Mwanamuziki wa Nigeria Burna Boy amejitokeza kukosoa mashabiki zake kwa jinsi wamepokea wimbo wake uitwao “Last Last”. Burna alifanya ufafanuzi huo kupitia akaunti yake rasmi ya mtandao wa Tik Tok ambapo alisema watu wanafurahia wakichezea wimbo huo ilhali ni wa kuvunjika moyo kutokana na mapenzi.


Huenda mwanamuziki huyo anapitia wakati mgumu kuhusiana na maswala ya mapenzi na kusababisha aandike na kuimba wimbo huo. Mwezi Januari mwaka huu alisema kwamba hataki tena kuwa na hisia kama binadamu na alikuwa tayari kulipa kiasi chochote cha fedha kwa yeyote ambaye angesaidia kumwondolea hisia.


Lawama zake ziliambatanishwa na tukio la mwanamuziki huyo kuachana na mpenzi wake Stefflon Don ambaye pia ni mwanamuziki wa nchini Uingereza. Uvumi kuhusu kutengana kwa wawili hao ulisheheni mitandaoni mwezi Disemba mwaka 2021 na siku chache baadaye Burna Boy akathibitisha kupitia Instagram ambapo aliandika kwamba yeye hana mke.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments