Ticker

6/recent/ticker-posts

Mzee Mfinanga Aibuka Akidai ni Baba Mzazi wa Nandy, Asimulia Jinsi Alivyokutana na Mama Yake MzaziIKIWA ni siku chache baada ya mastaa wa Bongo Fleva, Faustina Charles Mfinanga maarufu kama Nandy na William Nicolaus Lyimo ‘Billnass’ kufunga ndoa, basi mzee mmoja ameibuka na kudai kuwa yeye ndiye baba mzazi wa Nandy.

Akizungumza katika mahojiano na chombo kimoja cha habari nchini, mzee huyo aliyejitambulisha kwa jina la Charles Godfrey Mfinanga amesema;

“Mimi naitwa Charles Godfrey Mfinanga, mama yake tulipotezana akiwa mjamzito. Nilikuwa mtu wa madini, sikuweza kumtafuta na wakati huo mwaka 1992 hakukuwa na simu kwa ajili ya mawasiliano.

“Nimeona nijitambulishe anikubali au anikatae lakini ajue kwamba mimi ndio baba yake wa kumzaa kama ana mwingine ni wa kumlea.


 
“Mimi na mama yake Nandy hatukuwa na tatizo lolote isipokuwa dada yake alimuonea wivu wakati nipo na yule mama. Akamtorosha/kumpoteza kama mfanyakazi akampeleka sehemu ambayo sijui.

“Nachotamani kumwambia Nandy ni kitu kimoja, mimi sijawahi kumuona, kama ametambua kuna Charles Mfinanga zaidi ya mimi awe huru nampa baraka zote lakini ajue ni damu yangu.

“Najulikana Arusha nzima, nikakutana na huyu mwanamke ambaye hata sasa hivi nikimuona amezeeka sijui ana hali gani kama akinitambua anitambue au akinikataa anikatae ila aelewe Nandy ni mtoto wangu kwa sababu aliondoka na ujauzito,” amesema Mzee Charles Godfrey Mfinanga.


Kwa upande wake, Nandy aka Mama Kijacho hajajibu chochote mpaka sasa kuhusu madai ya mzee huyo.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments